Monday, December 3, 2018
Home »
» Katibu Mkuu (UWT) ahamia rasmi Dodoma
Katibu Mkuu (UWT) ahamia rasmi Dodoma
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Queen Mulozi amehamia rasmi jijini Dodoma.
Amesisitiza kwamba wanachama wa jumuiya hiyo, wanatakiwa kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina yao na chama na serikali.
Akizungumza baada ya kupokewa jijini hapo, Mlozi amesema alifanya ziara katika ofisini mbalimbali ili kujitambulisha, ikiwemo Ofisi ya CCM mkoa ofisi ya CCM wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, lakini alifurahi kuona mshikamano mzuri uliopo mkoani huo.
Alisema mkoa huo ndio unaoongoza kwa umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya Chama na serikali na ndio siri pekee ya kuendelea kuimarisha chama na kutekekeza Ilani yake kikamilifu.
Mlozi aliwashukuru kwa mapokezi hayo na kuwataka wampe ushirikiano ili wote kwa pamoja waweze kufanikisha kukivusha chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Bora tutoke jasho la damu sasa kujipanga ili baadaye tutoke jasho jepesi na jeupe, hivyo tufanye kazi kwa bidii usiku na mchana bila kuchoka ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi kwa wakati," amesema Mlozi.
Amewataka kuhakikisha kuwa asilimia nne ya mikopo ya wanawake, asilimia nne vijana na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu, inawafikia wanawake wa CCM na wanachama wa UWT, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanawajenga na kukiimarisha Chama.
Mkuu wa wilaya wewe ni kijana mdogo, rais amekuamini, chapakazi usiogope vitisho," amesema.
Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi, alimkaribisha katibu mkuu huyo na kuahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yake na kwamba Dodoma ndio utaratibu wao.
Ninatambua chaguzi zilizoko mbele yetu, ninatambua na nina imani kuwa ushirikiano huu ukiendelea hakuna atakayewatoa kwenye mstari," amesema Katambi
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment