Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ametoa rai kwa askari na wazalendo wote nchini kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli katika kufanya mapinduzi ya kiuchumi na maendeleo kwa watanzania.
DC Katambi ameyasema hayo wakati akifunga zoezi la upigaji shabaha kwa silaha lililokuwa likifanywa na Jeshi la Akiba Dodoma linalosimamiwa na wakufunzi wabobevu wa Jeshi la Wananchi JWTZ mkoani humo.
Aliwaasa askari hao kuwa na nidhamu,ukakamavu, umakini katika uamuzi, kuzingatia na kutekeleza kila amri halali, kutumia nguvu inapobidi, matendo sahihi na wepesi wa matendo kwani hizo ndio sifa kubwa za Askari.
" Nawaomba mkihitimu mkapambane bila haya na kwa kufuata sheria hakikisheni mnazuia wale wote wenye nia ovu na Nchi yetu, wahujumu uchumi, wala rushwa na wakwepa kodi wasiwe sehemu yenu nyie mkawe wapiganaji wa kuhakikisha mnazuia hayo yote," amesema DC Katambi.
Wednesday, October 24, 2018
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment