Thursday, October 25, 2018
John Cena adai yupo tayari kufanyiwa upasuaji ili apate mtoto
Licha ya kupitia kwenye mahusiano na wanawake lukuki, Mwanamieleka maarufu duniani, John Cena ameonekana nafsi yake kufedheheka kwa kukosa mtoto.
John Cena (41) ambaye ameshapitia kwenye maisha ya ndoa kwa miaka minne na aliyekuwa mke wake wa ndoa Elizabeth Huberdeau, hajabahatika kupata mtoto jambo ambalo amekiri linamnyima raha.
“nimepitia kwenye mahusiano tofauti tofauti, lakini sijabahatika kupata mtoto. mwanzoni nilikuwa naangalia mwanamke nitakaye jenga naye familia lakini kwa sasa natamani zaidi kupata mtoto hata kwa njia ya upasuaji ikiwezekana,“ameeleza John Cena kwenye mahojiano yake na kipindi cha Today cha NBC.
Mwanzoni mwa mwaka huu John Cena alimvisha pete ya uchumba mcheza mieleka mwenzie Nikki Bella lakini miezi miwili baadae wakamwagana.
Katika maisha yake yote, John Cena hajawahi kupata mtoto na alishawahi kutamka wazi miaka ya nyuma kwamba hapendi watoto
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment