Mfanyabishara Mo Dewji.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa katika mahojiano yake na www.eatv.tv amesema kuwa wamemwongezea ulinzi mfanyabiashara huyo katika kipindi hiki ambacho bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio.
"Katika kipindi hiki ambacho bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwake, tumemuongezea ulinzi", amesema Mambosasa.
Mo Dewji alitekwa Alfajiri ya Oktoba 11, katika hoteli ya Colosseum iliyopo Osterbay jijini Dar es salaam na kupatikana baada ya siku tisa katika maeneo ya Gymkhana alikotelekezwa na watekaji, huku pia wakitelekeza gari aina ya Toyota Surf walilolitumia likiwa na silaha kadhaa za moto.
0 comments:
Post a Comment