USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Kigogo UWT Kortini Kwa Kugushi Cheti cha Ndoa

Nora Mzeru jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Ester Kyara alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kuwa  katika siku isiyojulikana jijini Dar, es Salaam, kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati wakati wakijua si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, alikana na ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya Sh 2milioni.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 21, mwaka huu
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL