USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Thursday, October 25, 2018

Mkuu wa Kitengo cha Usalama Posta atoweka


Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa muda wa siku nane.

 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika hilo, Joseph Ngowi, aliliambia Nipashe jana kuwa Mwamgabe hajaonekana ofisini kwake kwa muda mrefu na hakuna taarifa zozote zilizotolewa za kutofika ofisini.

Alisema baada ya jitihada za kumtafuta maeneo mbalimbali ikiwamo nyumbani kwake kushindikana, wameona ni busara kutangaza kwenye vyombo vya habari.

Ofisa huyo alisema wametoa taarifa kuwa anatakiwa kuhudhuria kikao cha nidhamu cha shirika hilo Novemba mosi, mwaka huu.

“Ameitwa kwenye kikao cha nidhamu kutokana na kutoonekana kazini na nyumbani, kikao hiki kinataka kumuhoji sababu ya kutoonekana kwake,” alisema.

Nipashe ilitaka kujua kama Mwamgabe anakabiliwa na tuhuma nyingine ndani ya shirika hilo, lakini Ngowi alisema hafahamu kama alikuwa na tuhuma zingine zozote.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana kwenye vyombo vya habari, Mwamgabe hajaonekana kazini na nyumbani kwa muda na hajulikani alipo.

“Baada ya jitihada za kukutafuta kushindikana kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja, tunakufahamisha popote ulipo uhudhurie kikao cha nidhamu kitakachofanyika Novemba mosi majira ya saa 4:00 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano ghorofa ya 12 Posta Makao Makuu kujibu tuhuma za kinidhamu zinazokukabili,” lilisomeka tangazo hilo.

Aidha, tangazo hilo limemtaarifu kiongozi huyo kuwa shirika litaendelea na kikao hicho cha nidhamu kama atashindwa kuhudhuria bila taarifa kwa mwajiri wake.

Matukio ya watu kupotea yamekuwa yakiongezeka na katika utafiti uliofanywa na ITV hivi karibuni, watoto walio chini ya miaka 18 wanaongoza kwenye matukio ya kupotea, kati ya watu 94 walioripotiwa kupotea ndani ya miezi mitatu, wenye umri huo ni 61.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa watu 33 ambao wana umri zaidi ya miaka 18 walioripotiwa kupotea, wanawake wakiwa 13 na wanaume 20.

Katika taarifa hiyo jumla ya matukio 94 ambayo yaliripotiwa ITV kati ya mwezi Julai hadi Septemba, yanaonyesha Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaopotea ambao walifikia 75 na wengine 18 wakitoka mikoa mingine,” ilisema taarifa hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL