USIKATE TAMAA WEWE NI MSHINDI

Recent News

Wednesday, October 24, 2018

'Msanii Hawa wa Diamond afanyiwa upasuaji salama'

Msanii wa muziki Bongo Hawa amefanyiwa upasuaji baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa moyo.

Meneja wa WCB, Babu Tale ambaye yupo nchini India ameeleza kuwa atarejea wiki ijayo baada ya matibabu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Asante Mungu mgonjwa amemaliza salama hivi ameshazinduka na madaktari wametupa uhakika wa mgonjwa atakua salama na mpaka hivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar," ameeleza.

"Hii ni hatua kubwa sana na mtihani unamkuta kila binadamu na mwenye kuutatua ni Mungu mwenyewe niwashukuru wote mlioweza kumuombea dua hawa mpaka hapa alipo na pia niendelee kuwaomba msiache kuomba dua," ameeleza Babu Tale.

Utakumbuka muimbaji Hawa alijizolea umaarufu mkubwa aliposhirikishwa na Diamond Platnumz kwenye wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nitarejea
Share:

0 comments:

Post a Comment

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Author Details

Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.

Followers

Search This Blog

Support

SUBSCRIBE OUR CHANEL