Klabu ya Singida United imeendelea kuwapoteza nyota wake baada ya wachezaji kadhaa kuondoka, ambapo sasa ni zamu ya Lubinda Mundia ambaye naye ameripotiwa kuachana na klabu hiyo.
Mundia ambaye ni mchezaji wa klabu ya Red Arrows ya Zambia alikuwa anachezea Singida United kwa mkopo hivyo amerejea kwenye timu yake baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Singida United imethibitisha kumalizana na mchezaji huyo ambaye ni askari wa zamani wa Jeshi la Anga nchini humo na tayari ameshatua kwenye klabu yake hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.
''Lubinda alikuwa mchezaji wetu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Red Arrows, amereja kuitumikia timu yake ya zamani baada ya mwaka mmoja wa mkopo kumalizika, tunamshukuru kwa huduma yake ambayo imekuwa na mafanikio kwetu'', amesema Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga.
Singida United sasa imeondokewa na nyota wake wanne msimu huu wa ligi ambao ni Lubinda Mundila, Peter Manyika Jr, Jamal Mwambeleko na Miraj Adam. Imeelezwa kuwa sababu ya kuondoka kwao ni kutotimiziwa stahiki zao ikiwemo mishahara na pesa za usajili.
Thursday, October 25, 2018
';
(function() {
var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true;
dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js';
(document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq);
})();
0 comments:
Post a Comment